Numbers 2:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya beramu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na marago ya Walawi katikati ya marago yote; kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hema la Mkutano na liondoke pamoja nao wakaao makambini kwa Walawi, liwe katikati ya makambi; kama walivyopanga makambini ndivyo waondoke kwenda kusafiri, kila mtu mahali pake penye bendera ya kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na marago ya Walawi katikati ya marago yote; kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, kambi ya kabila la Walawi likiwa katikati ya kambi zote nao wakibeba hilo hema la mukutano wataondoka; kila kundi likisafiri kwa kufuata nafasi yake kwa bendera.