Numbers 2:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni elfu mia moja na nane na mia moja. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wote waliohesabiwa katika marago ya Efraimu walikuwa mia na nane elfu na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri katika mahali pa tatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu walikuwa elfu mia moja na nane na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaoondoka wakiwa kundi la tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jumla yao wote watakaokuwa makambini kwa Efuraimu ni watu 108100 kwa vikosi vyao, nao ndio wa tatu watakaoondoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote waliohesabiwa katika marago ya Efraimu walikuwa mia na nane elfu na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri katika mahali pa tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jumla ya watu waliokuwa katika kambi ya Efuraimu kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja na nane na mia moja. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la tatu.