Numbers 2:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Walipiga kambi zao, kufuata bendera zao na walisafiri kila mmoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru Musa. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya beramu zao. Pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyopanga penye beramu zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Walipiga kambi zao, kufuata bendera zao na walisafiri kila mmoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu BWANA alichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu bwana alichomwamuru Musa. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwamuru Musa; ndivyo walivyojipanga kufuata bendera zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Walipiga kambi zao, kufuata bendera zao na walisafiri kila mmoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli wakayafanya yote; kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, walivyoyapiga makambi yao penye bendera zao, tena ndivyo, walivyoondoka kwenda kusafiri kila mtu na ndugu zake penye milango ya baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyopanga penye beramu zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama vile Yawe alivyomwamuru Musa. Wakapiga kambi zao, kufuata bendera zao na wakasafiri kila mumoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.