Numbers 2:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni elfu mia moja themanini na sita na mia nne. Wao watatangulia kuondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote waliohesabiwa katika marago ya Yuda walikuwa mia na themanini na sita elfu na mia nne, kwa majeshi yao. Hao ndio watakaosafiri mbele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kwanza kuondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote waliohesabiwa katika kambi ya Yuda walikuwa elfu mia moja themanini na sita na mia nne, kwa makundi yao. Hao ndio watakaotangulia mbele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jumla yao wote watakaokuwa makambini kwa Yuda ni watu 186400 kwa vikosi vyao, nao ndio wa kwanza watakaoondoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote waliohesabiwa katika marago ya Yuda walikuwa mia na themanini na sita elfu na mia nne, kwa majeshi yao. Hao ndio watakaosafiri mbele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja makumi nane na sita na mia ine. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.