Numbers 20:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: Je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa na Haruni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Musa akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose na Aroni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka katika mwamba huu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa na Haruni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Musa akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: Je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose na Haroni wakalikusanya kundi la watu mbele ya mwamba, akawaambia: Sikieni, ninyi msiotii! Itakuwaje? Tutaweza kuwatolea ninyi maji humu mwambani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Musa na Haruni wakawakusanya watu wote pamoja mbele ya jiwe, naye Musa akawaambia: Musikilize sasa, enyi waasi; tuwatokezee maji kutoka katika jiwe hili?