Numbers 20:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Mose na Aroni waliondoka kwenye umati wa watu, wakaenda kusimama kwenye mlango wa hema la mkutano, wakasujudu. Basi, utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa na Haruni wakaondoka pale kwenye kusanyiko hadi kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukawatokea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Mose na Aroni waliondoka kwenye umati wa watu, wakaenda kusimama kwenye mlango wa hema la mkutano, wakasujudu. Basi, utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa BWANA ukawatokea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa na Haruni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa bwana ukawatokea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hadi mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Mose na Aroni waliondoka kwenye umati wa watu, wakaenda kusimama kwenye mlango wa hema la mkutano, wakasujudu. Basi, utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukawatokea,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose na Haroni wakatoka hapo, walipokusanyika, wakaenda hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano; napo hapo, walipoanguka kifudifudi, utukufu wa Bwana ukawatokea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo, Musa na Haruni wakaondoka kwenye mukutano wa watu, wakaenda kusimama kwenye mulango wa hema la mukutano, wakainama uso mpaka chini. Basi, utukufu wa Yawe ukawatokea,