Numbers 20:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Twaa ile fimbo yako, kisha wewe na Aroni ndugu yako, muikusanye jumuiya yote ya watu. Halafu, mbele ya macho yao, uuambie mwamba ulio mbele ya macho yao utoe maji yake. Naam, utaufanya mwamba utoe maji, ili jumuiya nzima ya watu na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Haruni mkawakusanye watu wote. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Twaa ile fimbo yako, kisha wewe na Aroni ndugu yako, muikusanye jumuiya yote ya watu. Halafu, mbele ya macho yao, uuambie mwamba ulio mbele ya macho yao utoe maji yake. Naam, utaufanya mwamba utoe maji, ili jumuiya nzima ya watu na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Aroni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka katika huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Haruni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Twaa ile fimbo yako, kisha wewe na Aroni ndugu yako, muikusanye jumuiya yote ya watu. Halafu, mbele ya macho yao, uuambie mwamba ulio mbele ya macho yao utoe maji yake. Naam, utaufanya mwamba utoe maji, ili jumuiya nzima ya watu na mifugo yao waweze kunywa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ichukue ile fimbo! Kisha wewe na kaka yako Haroni wakusanyeni wao wote wa mkutano, mseme na mwamba huu machoni pao wote, ndipo, utakapowapa maji yake. Ndivyo, utakavyowatolea maji humu mwambani, uwanyweshe wao wa mkutano pamoja na nyama wao wa kufuga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Twaa ile fimbo yako, kisha wewe na ndugu yako Haruni mukusanye watu wote pamoja. Halafu, mbele ya macho yao, uambie jiwe linalokuwa mbele ya macho yao litoe maji yake. Utawatoshea maji ndani ya jiwe watu wote na mifugo yao waweze kunywa.