Numbers 21:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuiteka nchi yake yote mpaka mto Arnoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia, na akawa amechukua ardhi yake yote hadi Mto Arnoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuiteka nchi yake yote mpaka mto Arnoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuiteka nchi yake yote mpaka mto Arnoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Hesiboni ulikuwa mji wa Sihoni, mfalme wa Waamori; naye aliupigania kale na mfalme wa Moabu, ndipo, alipoichukua hiyo nchi yake na kuitoa mkononi mwake mpaka mto wa Arnoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hesiboni ulikuwa muji wa Sihoni mufalme wa Waamori, ambaye mbele alikuwa amepigana na mufalme wa Moabu na kuteka inchi yake yote mpaka muto Arnoni.