Numbers 21:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akalisikia ombi lao, akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Waisraeli wakawaangamiza kabisa Wakanaani pamoja na miji yao. Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Horma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasikiza sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akalisikia ombi lao, akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Waisraeli wakawaangamiza kabisa Wakanaani pamoja na miji yao. Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Horma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasikia sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akalisikia ombi lao, akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Waisraeli wakawaangamiza kabisa Wakanaani pamoja na miji yao. Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Horma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akazisikia sauti zao Waisiraeli, akawapa hao Wakanaani, nao wakawaangamiza wao pamoja na miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo; kwa hiyo wakapaita mahali pale Horma (Mwiko).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasikiza sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akasikia ombi lao, akawapa ushindi juu ya Wakanana. Waisraeli wakaangamiza kabisa Wakanana pamoja na miji yao. Kwa hiyo pahali pale pakaitwa Horma, ni kusema “Maangamizi”.