Numbers 21:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wakamwendea Mose, wakamwambia, “Tumetenda dhambi kwa kumnungunikia Mwenyezi-Mungu na wewe pia. Mwombe Mwenyezi-Mungu atuondolee nyoka hawa.” Kwa hiyo, Mose akawaombea watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wakamjia Musa na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya Mwenyezi Mungu na dhidi yako. Mwombe Mwenyezi Mungu ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Musa akawaombea hao watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wakamwendea Mose, wakamwambia, “Tumetenda dhambi kwa kumnung'unikia Mwenyezi-Mungu na wewe pia. Mwombe Mwenyezi-Mungu atuondolee nyoka hawa.” Kwa hiyo, Mose akawaombea watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya BWANA na dhidi yako. Mwombe BWANA ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wakamjia Musa na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya bwana na dhidi yako. Mwombe bwana ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Musa akawaombea hao watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wakamwendea Mose, wakamwambia, “Tumetenda dhambi kwa kumnungunikia Mwenyezi-Mungu na wewe pia. Mwombe Mwenyezi-Mungu atuondolee nyoka hawa.” Kwa hiyo, Mose akawaombea watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu walipomjia Mose, wakasema: Tumekosa tulipomgombeza Bwana, hata wewe. Tuombee kwake Bwana, awaondoe hawa nyoka kwetu! Mose alipowaombea hao watu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu wakamwendea Musa, wakamwambia: Tumetenda zambi kwa kumunungunikia Yawe na wewe vilevile. Umwombe Yawe atuondolee nyoka hawa. Kwa hiyo, Musa akawaombea watu.