Numbers 22:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Punda alipomwona malaika huyo wa Mwenyezi-Mungu, akajisukumiza ukutani na kuubana mguu wa Balaamu hapo. Kwa hiyo Balaamu akampiga tena huyo punda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Punda alipomwona malaika wa Mwenyezi Mungu, alijisukumiza karibu na ukuta, na kugandamiza mguu wa Balaamu ukutani. Ndipo Balaamu akampiga tena punda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Punda alipomwona malaika huyo wa Mwenyezi-Mungu, akajisukumiza ukutani na kuubana mguu wa Balaamu hapo. Kwa hiyo Balaamu akampiga tena huyo punda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Punda alipomwona malaika wa BWANA, alijisukumiza karibu na ukuta, na kugandamiza mguu wa Balaamu ukutani. Ndipo Balaamu akampiga tena punda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Punda alipomwona malaika wa bwana, alijisukumiza karibu na ukuta, na kugandamiza mguu wa Balaamu ukutani. Ndipo Balaamu akampiga tena punda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajisukuma ukutani, akaubana mguu wake Balaamu, basi akampiga mara ya pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Punda alipomwona malaika huyo wa Mwenyezi-Mungu, akajisukumiza ukutani na kuubana mguu wa Balaamu hapo. Kwa hiyo Balaamu akampiga tena huyo punda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Punda alipomwona malaika wa Bwana akajisonga ukutani na kuuchubua mguu wa Bileamu; ndipo, alipompiga tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Punda alipomwona malaika huyo wa Yawe, akajibanisha kwenye ukuta na kubana muguu wa Balamu hapo. Kwa hiyo Balamu akamupiga tena huyo punda.