Numbers 22:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Mwenyezi-Mungu akayafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama njiani, ameshika upanga uliochomolewa alani mwake. Balaamu akajitupa chini kifudifudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Mwenyezi Mungu amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Mwenyezi-Mungu akayafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama njiani, ameshika upanga uliochomolewa alani mwake. Balaamu akajitupa chini kifudifudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa bwana amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, akiwa na upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa, naye akainamisha kichwa, akaanguka kifudifudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Mwenyezi-Mungu akayafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Mwenyezi-Mungu amesimama njiani, ameshika upanga uliochomolewa alani mwake. Balaamu akajitupa chini kifudifudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipoyafumbua macho yake Bileamu, akamwona malaika wa Bwana, alivyosimama njiani na kushika mkononi upanga uliochomolewa; ndipo, alipomwinamia na kumwangukia kifudifudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo, Yawe akafungua macho ya Balamu, naye akamwona malaika wa Yawe amesimama katika njia, akishika upanga uliochomolewa toka kifuko chake. Balamu akajitupa uso mpaka chini.