Numbers 22:41 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake, Balaki alimchukua Balaamu, akapanda naye mpaka Bamoth-baali; kutoka huko, Balaamu aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi iliyofuata Balaki akamchukua Balaamu hadi Bamoth-Baali, na kutoka huko Balaamu akawaona baadhi ya watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake, Balaki alimchukua Balaamu, akapanda naye mpaka Bamoth-baali; kutoka huko, Balaamu aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi iliyofuata Balaki akamchukua Balaamu mpaka Bamothi Baali, na kutoka huko Balaamu akawaona baadhi ya watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi iliyofuata Balaki akamchukua Balaamu mpaka Bamoth-Baali, na kutoka huko Balaamu akawaona baadhi ya watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hadi Bamoth-baali; na kutoka huko aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli hadi pande zao za mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake, Balaki alimchukua Balaamu, akapanda naye mpaka Bamoth-baali; kutoka huko, Balaamu aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa asubuhi, Balaka akamchukua Bileamu, akampeleka juu vilimani kwa Baali; huko ndiko, alikowaona watu hao hata mwisho wa makambi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake, Balaki akamutwaa Balamu, akapanda naye mpaka Bamoti-Bali; kutoka huko, Balamu aliweza kuwaona wamoja kati ya Waisraeli.