Numbers 22:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akapeleka ujumbe kwa Balaamu, mwana wa Beori, huko Pethori, karibu na mto Eufrate, nchini Amawi. Alimwambia Balaamu hivi: “Kuna taifa ambalo limetoka Misri, nalo limeenea kila mahali nchini, tena linatishia kuchukua ardhi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akatuma wajumbe kwenda kumwita Balaamu mwana wa Beori, aliyekuwa huko Pethori, karibu na Mto, katika nchi yake ya kuzaliwa. Balaki akasema: “Taifa limekuja kutoka Misri, nao wamefunika uso wa nchi, nao wamekaa karibu nami.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akapeleka ujumbe kwa Balaamu, mwana wa Beori, huko Pethori, karibu na mto Eufrate, nchini Amawi. Alimwambia Balaamu hivi: “Kuna taifa ambalo limetoka Misri, nalo limeenea kila mahali nchini, tena linatishia kuchukua ardhi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akatuma wajumbe kwenda kumwita Balaamu mwana wa Beori, ambaye alikuwa huko Pethori, karibu na Mto Eufrati, katika nchi yake ya kuzaliwa. Balaki akasema: “Taifa limekuja kutoka Misri, nao wamefunika uso wa nchi, nao wametua karibu nami.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akatuma wajumbe kwenda kumwita Balaamu mwana wa Beori, ambaye alikuwa huko Pethori, karibu na Mto Frati, katika nchi yake ya kuzaliwa. Balaki akasema: “Taifa limekuja kutoka Misri, nao wamefunika uso wa nchi, nao wametua karibu nami.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hadi Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akapeleka ujumbe kwa Balaamu, mwana wa Beori, huko Pethori, karibu na mto Eufrate, nchini Amawi. Alimwambia Balaamu hivi: “Kuna taifa ambalo limetoka Misri, nalo limeenea kila mahali nchini, tena linatishia kuchukua ardhi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
alipotuma wajumbe kwenda Petori kwa Bileamu, mwana wa Beori, aliyekaa kwenye lile jito kubwa katika nchi yao walio ukoo wake, wamwite na kumwambia: Tazama, wako watu waliotoka Misri, nao wanaifunika nchi hii pote, unapotazama, tena wanakaa kunielekea mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akapeleka ujumbe kwa Balamu mwana wa Beori, huko Petori, karibu na muto Furati katika inchi ya Amawi. Akamwambia Balamu hivi: Kuna taifa ambalo limetoka Misri, nalo limeenea kila pahali katika inchi, tena linatishia kutwaa inchi yangu.