Numbers 23:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Balaki akamchukua Balaamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Hapo akajenga madhabahu saba na kutoa juu ya kila madhabahu kafara ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamchukua mpaka shamba la Sofimu, hata kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Balaki akamchukua Balaamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Hapo akajenga madhabahu saba na kutoa juu ya kila madhabahu kafara ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamchukua mpaka shamba la Sofimu, hadi kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka ng'ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Balaki akamchukua Balaamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Hapo akajenga madhabahu saba na kutoa juu ya kila madhabahu kafara ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamchukua, akampeleka juu mlimani kwa Pisiga kulikokuwa uwanda wa wachunguliaji. Huko nako akajenga mahali saba pa kutambikia, kisha akatoa kila mahali pa kutambikia ng'ombe mmoja na kondoo mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamchukua mpaka shamba la Sofimu, hata kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Balaki akamutwaa Balamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha mulima Pisiga. Hapo akajenga mazabahu saba na kutoa juu ya kila mazabahu ngombe dume mumoja na kondoo dume mumoja.