Numbers 23:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je, Mwenyezi Mungu amesema nini?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, Bwana amenena nini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Je, BWANA amesema nini?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je, bwana amesema nini?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, BWANA amenena nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliporudi kwake akamwona, akisimama penye ng'ombe yake ya tambiko pamoja na wakuu wote wa Moabu. Balaka alipomwuliza: Bwana amesema nini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, BWANA amenena nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Balamu akarudi, akamukuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na wakubwa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza: Yawe amekuambia nini?