Numbers 23:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo, wala udhia kwa hao wana wa Israeli. Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao, yeye huzipokea sifa zao za kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. Mwenyezi Mungu, Mungu wao, yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo kati yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo, wala udhia kwa hao wana wa Israeli. Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao, yeye huzipokea sifa zao za kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. BWANA, Mungu wao yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. bwana, Mungu wao yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme iko katikati yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo, wala udhia kwa hao wana wa Israeli. Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao, yeye huzipokea sifa zao za kifalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna aliyepata kutazama mambo yaliyo ya bure kwake Yakobo, wala hakuna aliyeona masumbuko kwake Isiraeli; Bwana Mungu wake yuko pamoja naye, nayo mashangilio ya mfalme husikilika kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe hajaona ubaya kwa watu wa Yakobo, wala uovu kwa hao watu wa Israeli. Yawe Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye anasifiwa kwa vigelegele kati yao, yeye anapokea sifa zao za kifalme.