Numbers 23:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninaenda kando. Huenda Mwenyezi Mungu atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda Bwana atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda BWANA atakuja kukutana nami. Lo lote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda bwana atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lolote atakalonionesha nitakuambia. Akaenda hadi mahali peupe juu ya kilima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bileamu akamwambia Balaka: Simama penye ng'ombe yako ya tambiko! Lakini mimi nitakwenda, labda Bwana atakuja kunikuta; ndipo, nitakapokuambia hilo neno, atakalonionyesha. Kisha akaenda kilimani palipo peupe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Balamu akamwambia Balaki: Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa kwa moto, nami niende. Labda Yawe atakutana nami. Chochote atakachonionyesha nitakuja kukuambia. Basi, Balamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mulima.