Numbers 24:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu, nami imenipasa kusema tu kile Mwenyezi Mungu atakachosema’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; Bwana atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu cho chote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la BWANA, nami imenipasa kusema tu kile BWANA atakachosema’?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la bwana, nami imenipasa kusema tu kile bwana atakachosema’?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ijapo Balaka anipe nyumba yake ijaayo fedha na dhahabu, sitaweza kukipita kinywa cha Bwana, nifanye jambo baya au jema, kama moyo wangu unavyotaka; ila Bwana atakaloniambia, ndilo hilo, nitakalolisema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwaambia kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa feza na zahabu, mimi sitaweza kubadilisha agizo la Yawe, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa mapenzi yangu mwenyewe. Nilisema kwamba atakachosema Yawe ndicho nitakachosema.