Numbers 25:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue hadharani mbele za Mwenyezi Mungu, ili hasira kali ya Mwenyezi Mungu iweze kuondoka kwa Israeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamwambia Mose, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele za BWANA, ili hasira kali ya BWANA iweze kuondoka kwa Israeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamwambia Musa, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele za bwana, ili hasira kali ya bwana iweze kuondoka kwa Israeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele za BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose: Wachukue wakuu wote wa watu hawa, uwanyonge juani mbele ya Bwana, haya makali ya Bwana yawakayo moto yapate kupoa na kuwaondokea Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie BWANA watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akamwambia Musa: Utwae viongozi wote wa Israeli, uwatundike mbele yangu jua kati, kusudi kasirani yangu juu yenu ipite.