Numbers 26:63 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ng’ambo ya Yeriko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati walipowahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng'ambo ya Yeriko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao ndio wanaume Waisraeli walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii ndiyo jumla yao, Mose na mtambikaji Elazari waliowakagua, walipowakagua wana wa Isiraeli kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao ndio wanaume Waisraeli waliohesabiwa na Musa na kuhani Eleazari katika inchi za mabonde za Moabu, ngambo ya muto Yordani, karibu na Yeriko.