Numbers 26:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tatu mia saba na thelathini (43,730).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arobaini na tatu, mia saba na thelathini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizi ndizo ndugu zao Warubeni, nao wa kwao waliokaguliwa walikuwa watu 43730.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hizo ndizo ukoo za kabila la Rubeni. Hesabu ya wanaume waliohesabiwa ni elfu makumi ine na tatu, mia saba na makumi tatu.