Numbers 28:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwanzoni mwa kila mwezi, mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa: Fahali wadogo wawili, kondoo dume mmoja na, wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Mwenyezi Mungu sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwanzoni mwa kila mwezi, mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa: fahali wadogo wawili, kondoo dume mmoja na, wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea BWANA sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe dume wadogo wawili, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja, wakamilifu, saba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwanzoni mwa kila mwezi, mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa: Fahali wadogo wawili, kondoo dume mmoja na, wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena siku za kwanza za miezi yenu na mmtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima: madume mawili ya ng'ombe walio vijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mwanzo wa kila mwezi, mutamutolea Yawe sadaka ya kuteketezwa: wana-ngombe dume wawili, kondoo dume mumoja, wana-kondoo dume saba wa mwaka mumoja, wasiokuwa na kilema.