Numbers 28:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa BWANA kama sadaka ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa bwana kama sadaka ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku Bwana na atolewe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na kinywaji chake cha tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena mutamutolea Yawe sadaka kwa ajili ya zambi, beberu mumoja, zaidi ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.