Numbers 28:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku ya Sabato, mtatoa sadaka ya wanakondoo wawili wa kiume wa mwaka mmoja wasio na dosari, sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku ya Sabato, mtatoa sadaka ya wanakondoo wawili wa kiume wa mwaka mmoja wasio na dosari, sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo dume wawili, wa mwaka mmoja, wakamilifu, pamoja na sehemu ya mbili ya kumi za efa za unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku ya Sabato, mtatoa sadaka ya wanakondoo wawili wa kiume wa mwaka mmoja wasio na dosari, sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena siku ya mapumziko mtoe wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na kilema na vibaba sita vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko, tena kinywaji chake cha tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya Sabato, mutatoa sadaka ya wana-kondoo dume wawili wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema, sadaka ya vyakula ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.