Numbers 29:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya weuo ya sikukuu ya Mapoza na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao ya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatoa vilevile beberu mumoja kwa sadaka kwa ajili ya zambi zaidi ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya vyakula na sadaka zake za kinywaji.