Numbers 29:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga kumi na watatu, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja. Wote wawe bila dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng'ombe waume wadogo kumi na watatu, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: fahali wachanga kumi na watatu, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja. Wote wawe bila dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume wachanga kumi na watatu na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, iliyo harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga kumi na watatu, kondoo madume wawili, wanakondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja. Wote wawe bila dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo na mtoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana: madume kumi na matatu ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe waume wadogo kumi na watatu, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, yenye harufu nzuri inayomupendeza Yawe: wana-ngombe dume kumi na watatu, kondoo dume wawili, wana-kondoo kumi na wane wa mwaka mumoja. Wote wasikuwe na kilema.