Numbers 29:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sadaka itakayoandamana nazo itakuwa unga safi uliochanganywa na mafuta: Kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng'ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya kumi mbili kwa kila kondoo katika hao kondoo waume wawili;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sadaka itakayoandamana nazo itakuwa unga safi uliochanganywa na mafuta: kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo waume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa kila ng'ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya mbili ya kumi kwa kila kondoo katika hao kondoo dume wawili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sadaka itakayoandamana nazo itakuwa unga safi uliochanganywa na mafuta: Kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe wa wale madume ya ng'ombe kumi na matatu na vibaba sita vya dume moja la kondoo wa wale madume mawili ya kondoo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya kumi mbili kwa kila kondoo katika hao kondoo waume wawili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sadaka itakayoandamana nazo itakuwa unga safi uliochanganywa na mafuta: kilo tatu kwa kila ngombe dume, kilo mbili kwa kila kondoo,