Numbers 29:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku ya pili mtatoa: Fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Katika siku ya pili, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena siku ya pili mtasongeza ng'ombe waume wadogo kumi na wawili, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne wakamilifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku ya pili mtatoa: fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena siku ya pili mtasongeza ng'ombe dume wachanga kumi na wawili, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne wakamilifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku ya pili mtatoa: Fahali wachanga kumi na wawili, kondoo madume wawili, wanakondoo wa kiume kumi na wanne, wa mwaka mmoja wasio na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya pili na mtoe madume kumi na mawili ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena siku ya pili mtasongeza ng’ombe waume wadogo kumi na wawili, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne wakamilifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya pili mutatoa: wana-ngombe dume kumi na wawili, kondoo dume wawili, wana-kondoo dume kumi na wane, wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema.