Numbers 29:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Katika siku ya saba, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena siku ya saba mtasongeza ng'ombe waume saba, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena siku ya saba mtasongeza ng'ombe dume saba, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku ya saba mtatoa fahali saba, kondoo madume watatu, wanakondoo madume kumi na wanne wa mwaka mmoja, wasio na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya saba na mtoe madume saba ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena siku ya saba mtasongeza ng’ombe waume saba, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya saba mutatoa ngombe dume saba, kondoo dume watatu, wana-kondoo dume kumi na wane wa mwaka mumoja, wasiokuwa na kilema.