Numbers 29:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya ndiyo maagizo kuhusu sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na sadaka za amani mtakazomtolea Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Licha ya hizi zote, zipo pia sadaka za kuteketezwa, za nafaka na za kinywaji, ambazo mnamtolea Mwenyezi-Mungu kutimiza nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sadaka hizo mtamsongezea Bwana katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya ndiyo maagizo kuhusu sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na sadaka za amani mtakazomtolea Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Licha ya hizi zote, zipo pia sadaka za kuteketezwa, za nafaka na za kinywaji, ambazo mnamtolea Mwenyezi-Mungu kutimiza nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya BWANA kwenye sikukuu zenu zilizoamuriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya bwana kwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sadaka hizo mtamsogezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya ndiyo maagizo kuhusu sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na sadaka za amani mtakazomtolea Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Licha ya hizi zote, zipo pia sadaka za kuteketezwa, za nafaka na za kinywaji, ambazo mnamtolea Mwenyezi-Mungu kutimiza nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizo ndizo ng'ombe za tambiko, mtakazomtolea Bwana, sikukuu zenu zitakapotimia; tena ziko zile, mtakazozitoa kwa kuapa au kwa kupenda wenyewe kuwa ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima au vilaji au vinywaji vyenu vya tambiko au ng'ombe zenu za tambiko za shukrani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sadaka hizo mtamsongezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo maagizo juu ya sadaka mutakazomutolea Yawe wakati wa sikukuu zenu zilizopangwa. Zaidi ya hizi zote, kuna vilevile sadaka za kuteketezwa, za vyakula na za kinywaji, za kutimiza kiapo na za mapenzi, na za amani.