Numbers 29:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mpya na sadaka yake ya nafaka, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji kama inavyotakiwa kuwa harufu nzuri ipendezayo, ni sadaka kwa Mwenyezi-Mungu iliyoteketezwa kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku, pamoja na sadaka zake za nafaka, na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, harufu inayopendeza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mpya na sadaka yake ya nafaka, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji kama inavyotakiwa kuwa harufu nzuri ipendezayo, ni sadaka kwa Mwenyezi-Mungu iliyoteketezwa kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa BWANA kwa moto, harufu inayopendeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa bwana kwa moto, harufu inayopendeza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mpya na sadaka yake ya nafaka, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji kama inavyotakiwa kuwa harufu nzuri ipendezayo, ni sadaka kwa Mwenyezi-Mungu iliyoteketezwa kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao na mtoe pamoja na ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima za mwandamo wa mwezi pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao vya tambiko, kama ilivyo desturi yao kuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatoa vitu hivi zaidi ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mupya na sadaka yake ya vyakula, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya vyakula na sadaka zake za kinywaji kama vile inavyoagizwa. Itakuwa harufu nzuri yenye kupendeza; ni sadaka kwa Yawe iliyoteketezwa kwa moto.