Numbers 29:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo saba wa mwaka mmoja. Wote wasiwe na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo saba wa mwaka mmoja. Wote wasiwe na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja; watakuwa wakamilifu kwenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo saba wa mwaka mmoja. Wote wasiwe na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila mtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza: dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutamutolea Yawe sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumupendeza Yawe: mwana-ngombe mumoja, kondoo dume mumoja, wana-kondoo saba wa mwaka mumoja. Wote wasikuwe na kilema.