Numbers 3:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose na Aroni na wana wao walitakiwa kupiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua. Wajibu wao ulikuwa kutoa huduma kwenye mahali patakatifu kwa lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyesogea karibu ilibidi auawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa, na Haruni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose na Aroni na wana wao walitakiwa kupiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua. Wajibu wao ulikuwa kutoa huduma kwenye mahali patakatifu kwa lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyesogea karibu ilibidi auawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea maawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine ye yote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa, na Haruni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea mawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose na Aroni na wana wao walitakiwa kupiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua. Wajibu wao ulikuwa kutoa huduma kwenye mahali patakatifu kwa lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyesogea karibu ilibidi auawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao waliopiga makambi mbele ya Kao upande wa mashariki, ndio mbele ya Hema la Mkutano upande wa maawioni kwa jua walikuwa Mose na Haroni na wanawe waliongoja zamu za kupaangalia Patakatifu mahali pao wana wa Isiraeli. Lakini mgeni aliyejitia katika kazi hizi hakuwa na budi kuuawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa na Haruni na wana wao watapiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki, ni kusema mbele ya hema la mukutano kuelekea upande linakotokea jua. Kazi yao itakuwa kutumika kwenye Pahali Patakatifu kwa jambo lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mutu mwingine yeyote aliyesogea karibu alipaswa kuuawa.