Numbers 3:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Idadi ya Walawi kulingana na familia zao, wanaume wote kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ambao Mose na Aroni waliwahesabu kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, ilikuwa watu 22,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Musa na Haruni kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kufuatana na koo zao, pamoja na kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa elfu ishirini na mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana, kwa jamaa zao, waume wote tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa ishirini na mbili elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Idadi ya Walawi kulingana na familia zao, wanaume wote kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ambao Mose na Aroni waliwahesabu kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, ilikuwa watu 22,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri ya BWANA, kufuatana na koo, pamoja na kila mwanaume mwenye mwezi mmoja au zaidi walikuwa 22,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Musa na Haruni kwa amri ya bwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa 22,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa jamaa zao, wanaume wote kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu ishirini na mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Idadi ya Walawi kulingana na familia zao, wanaume wote kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ambao Mose na Aroni waliwahesabu kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, ilikuwa watu 22,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jumla yao Walawi wote, Mose na Haroni waliowakagua kwa amri ya Bwana, waume wote wenye mwezi mmoja na zaidi wa udugu wao walikuwa watu 22000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa jamaa zao, waume wote tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa ishirini na mbili elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hesabu ya Walawi kulingana na jamaa zao, wanaume wote kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mumoja na zaidi ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Yawe, ilikuwa watu elfu makumi mbili na mbili.