Numbers 3:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakati walipomtolea Mwenyezi-Mungu moto usio mtakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakuwa na watoto kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakawa wanahudumu kama makuhani wakati wa uhai wa Aroni baba yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Mwenyezi Mungu walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Haruni baba yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana, waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana, katika bara ya Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani mbele ya uso wa Haruni baba yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakati walipomtolea Mwenyezi-Mungu moto usio mtakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakuwa na watoto kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakawa wanahudumu kama makuhani wakati wa uhai wa Aroni baba yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA wakati walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari peke yao walihudumu kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Haruni baba yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA, katika jangwa la Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani wakati wa uhai wa Haruni baba yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakati walipomtolea Mwenyezi-Mungu moto usio mtakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakuwa na watoto kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakawa wanahudumu kama makuhani wakati wa uhai wa Aroni baba yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Bwana walipomtolea Bwana moto mgeni wa mavukizo nyikani kwa Sinai, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo Elazari na Itamari walifanya kazi ya utambikaji na kuangaliwa na baba yao Haroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA, katika bara ya Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani mbele ya uso wa Haruni baba yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Yawe, wakati walipomutolea Yawe moto usiokuwa mutakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakukuwa na watoto. Kwa hiyo Eleazari na Itamari wakatumika kama vile makuhani chini ya uongozi wa baba yao Haruni.