Numbers 3:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe utatenga Walawi kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu; pia utatenga kwa ajili yangu mifugo yote ya Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo ya watu wa Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utawatwaa Walawi kwa ajili yangu mimi (Mimi ndimi Bwana) badala ya hao wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli; na wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe utatenga Walawi kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu; pia utatenga kwa ajili yangu mifugo yote ya Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo ya watu wa Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utawatwaa Walawi kwa ajili yangu mimi (Mimi ndimi BWANA) badala ya hao wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli; na wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe utatenga Walawi kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu; pia utatenga kwa ajili yangu mifugo yote ya Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo ya watu wa Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uwachukue Walawi kuwa wangu mimi Bwana, wakiwakomboa wana wote wa kwanza kwa wana wa Isiraeli, nao nyama wa kufuga wa Walawi na wawakomboe wana wa kwanza wa nyama wa kufuga wa wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utawatwaa Walawi kwa ajili yangu mimi (Mimi ndimi BWANA) badala ya hao wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli; na wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe utatenga Walawi kwa ajili yangu mimi Yawe; vilevile utatenga kwa ajili yangu mifugo yote ya Walawi pahali pa wazaliwa wa kwanza wa ngombe za watu wa Israeli.