Numbers 30:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama mumewe atakaposikia habari zake, akizitangua na kuzibatilisha, basi, hata kama alitaka kutimiza nadhiri au ahadi zake, hatawajibika kuzitimiza; mumewe atakuwa amezitangua na Mwenyezi-Mungu atamsamehe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zozote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, na Mwenyezi Mungu atamweka huru yule mwanamke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na Bwana atamsamehe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kisha mume wake akasikia jambo hilo lakini asimpinge, wala kumwambia kitu, basi, nadhiri zake zote zitambana; kadhalika na ahadi zake zote zitambana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zo zote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, na BWANA atamweka huru yule mwanamke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zozote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, na bwana atamweka huru yule mwanamke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na BWANA atamsamehe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama mumewe atakaposikia habari zake, akizitangua na kuzibatilisha, basi, hata kama alitaka kutimiza nadhiri au ahadi zake, hatawajibika kuzitimiza; mumewe atakuwa amezitangua na Mwenyezi-Mungu atamsamehe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mumewe akivitangua kabisa siku hiyo, anapopata habari, basi, yote yaliyotoka midomoni mwa mkewe ya kiapo nayo ya kujifungia kifungo hayatakuwapo, kwa kuwa mumewe ameyatangua, naye Bwana atamwondolea jambo hilo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na BWANA atamsamehe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kisha mume wake akisikia jambo hilo naye hamupingi, wala kumwambia kitu, basi, viapo vyake vyote vitamufunga; vilevile na ahadi zake zote zitamufunga.