Numbers 30:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa mumewe hatasema neno lolote tangu siku atakaposikia habari za nadhiri au ahadi za mkewe, basi atakuwa amezithibitisha siku hiyo alipopata habari zake kwa sababu hakusema chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa mumewe hasemi lolote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lolote kwa mkewe anapoyasikia hayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri au ahadi yoyote inayomfunga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa mumewe hasemi lo lote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lo lote kwa mkewe anapoyasikia hayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa mumewe hasemi lolote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lolote kwa mkewe anapoyasikia hayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa mumewe hatasema neno lolote tangu siku atakaposikia habari za nadhiri au ahadi za mkewe, basi atakuwa amezithibitisha siku hiyo alipopata habari zake kwa sababu hakusema chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mumewe akimnyamazia kimya tangu leo hata kesho, basi, amekwisha kuyatia nguvu, yawepo yote, aliyoyaapa, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, amekwisha kuvitia nguvu navyo, viwepo, kwani amemnyamazia kimya siku hiyo, alipopata habari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mume wake anaweza kuhakikisha au kufunga kiapo au ahadi yoyote inayomufunga.