Numbers 30:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hizi ndizo kanuni ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya mume na mkewe; baba na binti yake, huyo binti akiwa bado kijana na anakaa nyumbani kwa baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio masharti ambayo Mwenyezi Mungu alimpa Musa kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani mwa baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hizi ndizo amri, ambazo Bwana alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini akizibatilisha na kuzitangua muda fulani baada ya kusikia habari zake, basi yeye atakuwa na lawama kwa kosa la mkewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo masharti ambayo BWANA alimpa Mose kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo masharti ambayo bwana alimpa Musa kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hizi ndizo amri, ambazo BWANA alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, akiwa nyumbani mwa babaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hizi ndizo kanuni ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya mume na mkewe; baba na binti yake, huyo binti akiwa bado kijana na anakaa nyumbani kwa baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo maongozi, Bwana aliyomwagiza Mose ya kuwaongoza mtu na mkewe, hata baba na mwanawe wa kike, akiwa angaliko kijana na kukaa nyumbani mwa baba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hizi ndizo amri, ambazo BWANA alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akiifunga na kuivunja muda fulani nyuma ya kusikia habari yake, basi yeye atabeba lazima ya kosa la muke wake.