Numbers 30:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanaume awekapo nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mose alizungumza na viongozi wa makabila ya Israeli, akawaambia, “Hili ndilo neno lililoamriwa na Mwenyezi-Mungu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mwanaume awekapo nadhiri kwa BWANA, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanaume awekapo nadhiri kwa bwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akimwapia Bwana kumtolea cho chote au kiapo cha kujifungia kifungo cho chote, asilitangue neno lake, ila sharti ayafanye yote, kama kinywa chake kilivyoyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Musa akazungumuza na viongozi wa makabila ya Israeli, akawaambia: Hili ndilo neno lililoamriwa na Yawe: