Numbers 30:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama baba yake akisikia juu ya nadhiri hiyo, akampinga, basi nadhiri zake na ahadi yake havitambana. Mwenyezi-Mungu atamsamehe kwa sababu baba yake amelipinga jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake yoyote aliyojifunga kwayo itakayosimama; Mwenyezi Mungu atamweka huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na Bwana atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na baba yake akawa amesikia ahadi hiyo, asimpinge, basi, nadhiri zake alizoweka zitambana na kila ahadi aliyotoa itambana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake ye yote aliyojifunga kwayo itakayosimama; BWANA atamwacha huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake yoyote aliyojifunga kwayo itakayosimama; bwana atamweka huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na BWANA atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama baba yake akisikia juu ya nadhiri hiyo, akampinga, basi nadhiri zake na ahadi yake havitambana. Mwenyezi-Mungu atamsamehe kwa sababu baba yake amelipinga jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini baba yake akimkataza siku hiyo, anapopata habari, basi, yote aliyoyaapa navyo vifungo vyote, alivyojifungia, havitakuwapo, naye Bwana atamwondolea jambo hilo, kwa kuwa baba yake amemkataza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na BWANA atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na baba yake akisikia ahadi hiyo naye hamupingi, yule binti atafungwa na kila kiapo na ahadi aliyofanya.