Numbers 30:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini nadhiri au ahadi yoyote aliyoiweka mama mjane au mwanamke aliyepewa talaka ambayo kwayo amejifunga, ni lazima imbane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nadhiri yoyote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachwa vitakuwa vimemfunga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama mume wake akisikia jambo hilo akampinga, basi huyo mumewe atabatilisha nadhiri ya mkewe na tamko lake alilotoa bila kufikiri; naye Mwenyezi-Mungu atamsamehe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nadhiri yo yote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachika vitakuwa vimemfunga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nadhiri yoyote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachwa vitakuwa vimemfunga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyetalikiwa, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini nadhiri au ahadi yoyote aliyoiweka mama mjane au mwanamke aliyepewa talaka ambayo kwayo amejifunga, ni lazima imbane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mjane au mwanamke aliyeachana na mumewe atakayoyaapa navyo vifungo vyote, atakavyojifungia, vitakuwapo, vimfunge.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama mume wake akisikia jambo hilo, akimupinga, basi huyo mume wake atavunja kiapo cha muke wake na maneno yale aliyosema bila kufikiri; naye Yawe atamusamehe.