Numbers 31:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakampelekea Mose na Eleazari, na jumuiya yote ya Waisraeli iliyokuwa kambini katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya Yordani karibu na Yeriko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Musa na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani, ng’ambo ya Yeriko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakampelekea Mose na Eleazari, na jumuiya yote ya Waisraeli iliyokuwa kambini katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya Yordani karibu na Yeriko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng'ambo ya Yeriko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Musa na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo kambini katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakampelekea Mose na Eleazari, na jumuiya yote ya Waisraeli iliyokuwa kambini katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya Yordani karibu na Yeriko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wote pia wakawapeleka kwa Mose na kwa mtambikaji Elazari na kwao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli; mateka na mapato ndiyo, waliyoyapeleka pamoja na nyara makambini kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani; ndipo hapo, Yeriko ulipokuwa ng'ambo ya pili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakamupelekea Musa na Eleazari, na Waisraeli wote waliokuwa katika kambi katika inchi za mabonde za Moabu, ngambo ya Yordani karibu na Yeriko.