Numbers 31:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose alikasirishwa na maofisa wa jeshi na makamanda waliosimamia makundi ya majeshi 1,000 na makundi ya wanajeshi mamia waliorudi kutoka vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose alikasirishwa na maofisa wa jeshi na makamanda waliosimamia makundi ya majeshi 1,000 na makundi ya wanajeshi mamia waliorudi kutoka vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, hao waliorudi kutoka kupigana vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose alikasirishwa na maofisa wa jeshi na makamanda waliosimamia makundi ya majeshi 1,000 na makundi ya wanajeshi mamia waliorudi kutoka vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mose akawakasirikia waliowekwa kuvisimamia vikosi, wale wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia waliotoka kwa kupiga vita;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akakasirikishwa na wakubwa wa jeshi na majemadari waliosimamia makundi ya waaskari elfu na makundi ya waaskari mamia waliorudi kutoka katika vita.