Numbers 31:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote wale walio miongoni mwenu ambao wameua mtu au kugusa maiti ni lazima wakae nje ya kambi kwa muda wa siku saba; jitakaseni pamoja na mateka wenu katika siku ya tatu na ya saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote wale walio miongoni mwenu ambao wameua mtu au kugusa maiti ni lazima wakae nje ya kambi kwa muda wa siku saba; jitakaseni pamoja na mateka wenu katika siku ya tatu na ya saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu ye yote au kumgusa mtu ye yote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya kambi muda wa siku saba; mtu yeyote aliyemwua mtu, na yeyote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote wale walio miongoni mwenu ambao wameua mtu au kugusa maiti ni lazima wakae nje ya kambi kwa muda wa siku saba; jitakaseni pamoja na mateka wenu katika siku ya tatu na ya saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha ninyi laleni nje ya makambi siku saba, ninyi nyote mlioua mtu nanyi mliogusa tu mtu aliyeuawa, mjieue siku ya tatu na siku ya saba, ninyi wenyewe pamoja na mateka yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote wale wanaokuwa kati yenu ambao wameua mutu au kugusa maiti wanapaswa kukaa inje ya kambi kwa muda wa siku saba; mujitakase pamoja na mateka wenu katika siku ya tatu na ya saba.