Numbers 31:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
yaani vitu vyote ambavyo vinastahimili moto, vitatakaswa kwa kupitishwa motoni. Hata hivyo, ni lazima vitakaswe kwa maji ya utakaso. Vitu vingine vyote ambavyo haviwezi kustahimili moto vitatakaswa kwa maji ya utakaso.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
yaani vitu vyote ambavyo vinastahimili moto, vitatakaswa kwa kupitishwa motoni. Hata hivyo, ni lazima vitakaswe kwa maji ya utakaso. Vitu vingine vyote ambavyo haviwezi kustahimili moto vitatakaswa kwa maji ya utakaso.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kitu kingine cho chote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu cho chote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya utakaso; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
yaani vitu vyote ambavyo vinastahimili moto, vitatakaswa kwa kupitishwa motoni. Hata hivyo, ni lazima vitakaswe kwa maji ya utakaso. Vitu vingine vyote ambavyo haviwezi kustahimili moto vitatakaswa kwa maji ya utakaso.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
navyo vyote vinavyoweza kuingia motoni sharti mvipitishe motoni, vipate kutakata, kisha mvieue kwa yale maji ya kunyunyiza; lakini vyote visivyopatana na moto na mvipitishe majini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ni kusema vitu vyote ambavyo vinavyovumilia moto, vitatakaswa kwa kupitishwa ndani ya moto. Hata hivyo, vinapaswa kutakaswa kwa maji ya utakaso. Vitu vingine vyote ambavyo haviwezi kuvumilia moto vitatakaswa kwa maji ya utakaso.