Numbers 31:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Mose akazungumza na watu akawaambia, “Watayarisheni watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kumlipizia Mwenyezi-Mungu kisasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Musa akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi Bwana, juu ya Midiani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Mose akazungumza na watu akawaambia, “Watayarisheni watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kumlipizia Mwenyezi-Mungu kisasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Musa akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipizia kisasi BWANA, juu ya Midiani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Mose akazungumza na watu akawaambia, “Watayarisheni watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kumlipizia Mwenyezi-Mungu kisasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Mose alipowaambia watu kwamba: Tengenezeni watu wa kwenu kwenda vitani, wawaendee Wamidiani kumpatia Bwana lipizo kwao Wamidiani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi BWANA, juu ya Midiani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Musa akazungumuza na watu akawaambia: Mutayarishe watu kwa vita waende kuwashambulia Wamidiani kwa kumulipizia Yawe kisasi.