Numbers 31:47 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya Bwana; kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama BWANA alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, wenye wajibu wa kuhudumu katika maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika nusu hii ya wana wa Isiraeli Mose akachukua mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, kama ni watu au nyama, akawapa Walawi waliongoja zamu ya kuliangalia Kao la Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya BWANA; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka nusu hii Waisraeli waliyopewa, Musa alitwaa mumoja kati ya kila mateka makumi tano na nyama makumi tano, kama alivyoamriwa na Yawe, akawapa Walawi ambao walitumika katika hema la Yawe.