Numbers 31:50 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tumeleta vyombo vya dhahabu, vikuku, bangili, pete za mhuri, vipuli na shanga ambavyo kila mtu alipata. Tumevitoa ili nafsi zetu zifanyiwe upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo tumeleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu ya vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi tumeleta matoleo ya Bwana, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tumeleta vyombo vya dhahabu, vikuku, bangili, pete za mhuri, vipuli na shanga ambavyo kila mtu alipata. Tumevitoa ili nafsi zetu zifanyiwe upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa BWANA vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za mhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tumeleta vyombo vya dhahabu, vikuku, bangili, pete za mhuri, vipuli na shanga ambavyo kila mtu alipata. Tumevitoa ili nafsi zetu zifanyiwe upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo tunamtolea Bwana vyombo vya dhahabu, kila mtu alivyoviona kuwa matoleo: vikuku na vitimbi na pete za vidoleni na mapete ya masikioni na mapambo yo yote, tujipatie upozi mbele ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, tumeleta vyombo vya zahabu, mikufu, vikomo, pete za muhuri, pete za masikio na ushanga ambavyo kila mutu alipata. Tumevitoa kusudi nafsi zetu zifanyiwe upatanisho mbele ya Yawe.